Tanzania yazindua mpango wa kuharakisha chanjo ya COVID-19
2021-09-16 09:33:23| cri

Katibu mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wa Tanzania Bw. Abel Makubi amesema kuwa Wizara ya afya ya Tanzania itazindua mpango unaolenga kuharakisha chanjo dhidi ya COVID-19.

Ameongeza kuwa mpango huo utakaoanza Septemba 20 utahusisha magari yanayotembea ya chanjo ili kufikia jamii zilizo kwenye maeneo ya mbali kote nchini, na idadi ya vituo vya chanjo ya COVID-19 itaongezeka hadi 6,784.

Amesema kuwa kuanzia tarehe 20 mwezi Septemba, watu laki 6 watapatiwa chanjo hiyo ndani ya wiki mbili.

Aidha Bw. Makubi aliwaagiza maafisa wa matibabu wa wilaya na mkoa kote nchini kusimamia utekelezaji wa mpango wa chanjo ya haraka ili kuwezesha watu wengi kupata chanjo kadiri iwezekanavyo.