Tatizo la uhaba wa chakula lawa kubwa zaidi nchini Sudan Kusini tangu ijipatie uhuru
2021-09-16 09:30:57| cri

Mkurugenzi wa Ofisi ya Uratibu wa Mambo ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa anayeshughulikia operesheni na matangazo Bibi Reena Ghelani jana alisema, watu wa Sudan Kusini wanakumbwa na kiwango cha juu zaidi cha uhaba wa chakula tangu nchi hiyo ijipatie uhuru kutoka Sudan miaka 10 iliyopita.

Amesema zaidi ya asilimia 60 ya watu wote takriban milioni 12.78 wa Sudan Kusini wanakumbwa na uhaba wa chakula. Masuala ya mapambano, changamoto za hali ya hewa, kukosa makazi, janga la Corona, ukosefu wa uwekezaji kwenye miundombinu na huduma za kimsingi yanawafanya watu hao wahitaji zaidi msaada. Kwa sasa, watu zaidi ya milioni 8.3 nchini humo wanahitaji msaada wa kibinadamu, ikiwa ni pamoja na watoto milioni 1.4.