EABC yataka kufanywa minyororo ya thamani iwe ya kidijitali ili kuongeza ushindani wa Afrika Mashariki
2021-09-17 10:23:17| cri

Baraza la Biashara la Afrika Mashariki (EABC) ambacho ni chombo cha sekta binafsi za kanda hii, limetaka kufanya minyororo ya thamani ya vifaa iwe ya kidijiti ili kukuza ushindani wa kiuchumi wa jumuiya hiyo.

Mwenyekiti wa EABC Bw. Nick Nesbitt amesema kuwa mfumo wa dijiti utawezesha biashara ya kanda hiyo kupanua mauzo ya nje kwenye eneo la Biashara Huria la Bara la Afrika (AfCFTA) na kukabiliana na athari za janga la COVID-19.

Ameongeza kuwa teknolojia za dijiti zinarahisisha usafirishaji wa EAC, sekta ya usafirishaji na vifaa itapunguza gharama ya kufanya biashara, kuboresha ushindani wa kuuza nje na kurahisisha usafirishaji wa mizigo kutoka bandarini, kwenye malori hadi kwa wateja.

Bw. Nesbitt akiongea wakati wa mkutano wa viongozi wa bahari wa Afrika Mashariki, amesema kuwa msongamano, ucheleweshaji, taratibu ngumu za kutoa kibali cha kusafirisha mizigo, uhifadhi duni na vituo vya kufunga gati ni miongoni mwa changamoto zinazokabili njia za uchukuzi za Afrika Mashariki.