Mjumbe wa China asema kitendo cha Marekani na Uingereza kuisaidia Australia kupata nyambizi ya nyuklia kitachangia kueneza nyukilia
2021-09-17 10:22:50| cri

Mjumbe wa China asema kitendo cha Marekani na Uingereza kuisaidia Australia kupata nyambizi ya nyuklia kitachangia kueneza nyukilia_fororder_VCG111348419589

Mjumbe wa China kwenye Umoja wa Mataifa Wang Qun ameeleza wasiwasi mkubwa wa China baada ya Marekani na Uingereza kutangaza kuisaidia Australia kupata nyambizi ya nyuklia.

Akihutubia kwenye mkutano wa Bodi ya Magavana wa Shirika la Nishati ya Atomiki Duniani (IAEA) Bw. Wang Qun na mashirika mengine ya kimataifa huko Vienna, wameelezea hatua hiyo ya nchi tatu kama “kitendo cha kueneza nyukilia waziwazi”. Marekani na Uingereza zote ni nchi zenye silaha za nyuklia, na ni mataifa yaliyomo kwenye mkataba unaopiga marufuku kueneza silaha za nyuklia (NPT), ambao unazuia uenezaji wa silaha na teknolojia za nyuklia, ikiwa ni jukumu la msingi kwa nchi zake wanachama.

Amesisitiza kuwa usaidizi kama huo wa wazi kwa Australia ni dhahiri utaongeza uenezaji wa vitu na teknolojia za nyuklia, jambo ambalo linapingana na malengo na majukumu ya msingi ya NPT.