Mawaziri wa mazingira wa Afrika wasisitiza tena kuunga mkono ufufukaji usiosababisha uchafuzi
2021-09-17 10:21:45| cri

Mawaziri wa mazingira wa nchi za Afrika wameahidi kufanya juhudi ya kuongeza rasilimali ili kuharakisha ufufukaji wa uchumi baada ya janga la Corona ambao hautasababisha uchafuzi.

Wakiongea jana kwenye mkutano wa 18 wa mawaziri wa mazingira wa Afrika (AMCEN), mawaziri hao wamesema sera za uungaji mkono, fedha za kutosha, nia njema ya kisiasa ni mambo muhimu katika kuiwekea Afrika kwenye njia ya ufufukaji endelevu na usiosababisha uchafuzi.

Waziri wa mazingira, misitu na uvuvi wa Afrika Kusini atakayemaliza muda wake wa uwenyekiti wa AMCEN Bibi Barbara Creecy amesema, kuimarisha uhifadhi wa makazi na kugharamia hali ya hewa vitasaidia ufufukaji huo. Ameongeza kuwa mazingira endelevu yanaweza kutumiwa kama kichocheo cha ufufukaji wa Afrika baada ya janga la Corona. Nchi za Afrika zinapaswa kutumia kichocheo cha kutoleta uchafuzi ili kurahisisha safari yake ya kuelekea kwenye ukuaji wenye kiwango cha chini cha kaboni.