Rais wa Somalia amvua madaraka waziri mkuu wakati mpasuko ukikua
2021-09-17 10:25:38| cri

Rais wa Somalia amvua madaraka waziri mkuu wakati mpasuko ukikua_fororder_VCG111255980674

Rais Mohamed Farmajo wa Somalia amemvua madaraka waziri mkuu Mohamed Roble, hatua ambayo itakuza mpasuko wa kisiasa kati ya viongozi hawa wawili.

Rais Farmajo alisema kwenye taarifa yake kuwa “amesitisha kwa muda” madaraka ya waziri mkuu huyu ya kuwaajiri na kuwaondoa maofisa wa serikali nchini humo.

Farmajo, ambaye amekuwa na mgogoro na Roble kuhusu kuendesha shughuli za serikali alimshutumu waziri mkuu huyu kwa kufanya maamuzi ya haraka na ya upande mmoja bila ya kushauriana kwanza na Ikulu ya rais. Pia amemkosoa Roble kwa kutotekeleza majukumu yake ya kuongoza mchakato wa uchaguzi, akisema maamuzi yake ya haraka yanaweza kusababisha misukosuko ya kisiasa na kiusalama nchini humo.