ECOWAS kupata ufumbuzi wa kudumu wa mgogoro wa kisiasa nchini Guinea
2021-09-17 10:24:23| cri

Viongozi wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Magharibi mwa Afrika ECOWAS wameanza mkutano muhimu wa kilele kuhusu mapinduzi ya kijeshi yaliyotokea nchini Guinea.

Huu ni mkutano wa pili wa viongozi wa jumuiya hiyo tokea Septemba 15.

Mwenyekiti wa ECOWAS Nana Akufo-Addo amesema ana imani kuwa jumuiya hiyo itapata ufumbuzi wa kudumu wa mgogoro wa kisiasa nchini Guinea, na kwamba ufumbuzi huo ni muhimu kuhakikisha utulivu wa kisiasa, amani na umoja wa eneo hilo.

Pia amesisitiza kuwa jumuiya hiyo inalaani mapinduzi yaliyotokea nchini Guinea, na kuzuiliwa kwa rais wa Guinea Alpha Conde.

Viongozi wa jumuiya hiyo walifanya mkutano wao wa kwanza juu ya mapinduzi ya Guinea Ijumaa iliyopita kwa njia ya video, ambapo walisitisha uanachama wa Guinea katika jumuiya hiyo, wakiitaka irejee mapema katika utaratibu wa kikatiba.