Balozi wa China kwenye UM asema utambuzi wa kimataifa wa haki ya maendeleo uko mbali sana
2021-09-17 10:22:21| cri

Mwakilishi wa Kudumu kwenye Ofisi ya Umoja wa Mataifa Geneva, Chen Xu amesema haki ya maendeleo ni haki ya binadamu duniani ambayo haipaswi kunyimwa, hata hivyo amesema kwa sasa utambuzi wa haki hiyo duniani uko mbali sana ambao ni chini ya matarajio.

Hayo ameyasema jana wakati akitoa taarifa ya pamoja kwa niaba ya zaidi ya nchi 50 kwenye Mkutano wa 48 wa Baraza la Haki za Binadamu, akitoa wito kwa vyombo vya haki za binadamu vya UM kutoa kipaumbele kwenye haki ya maendeleo na kuiingiza kwenye mfumo wa UM. Akizungumzia kuhusu virusi vya Corona balozi Chen amesisitiza kuwa janga la UVIKO-19 limeathiri vibaya maendeleo ya uchumi na jamii na maisha ya watu wa nchi zote, hasa nchi zinazoendelea, kuzidisha hali ya kutokuwepo usawa na kuleta changamoto mpya katika kutimiza haki ya maendeleo. Hata hivyo ameshauri kuwa wakati dunia ikikabiliwa na changamoto hizi, inapaswa kufuatilia maendeleo yanayowalenga watu na kutimiza matarajio ya watu ya kuwa na maisha bora.