Shughuli za kuadhimisha miaka 90 tangu kutokea kwa Tukio la Septemba 18 lafanyika mjini Shenyang
2021-09-19 14:31:35| cri

Shughuli za kupiga kengele zilifanyika kwenye uwanja wa Jumba la Makumbusho ya Tukio la Septemba 18 mjini Shenyang, mkoani Liaoning, ili kuadhimisha miaka 90 tangu kutokea kwa tukio hilo. Mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China Bw. Zhao Leji alihudhuria shughuli hizo na kutoa hotuba.

Shughuli hizo zilianza rasmi saa tatu asubuhi. Watu wote waliimba wimbo wa taifa. Baada ya hapo Bw. Zhao alitoa hotuba akisema kufanya shughuli za kupiga kengele ni kwa ajili ya kuwakumbusha watu historia ya tukio hilo, kuwakumbuka mashujaa waliotoa muhanga, kuenzi moyo wa kupambana na maadui, na kujenga mustakabali mzuri.