Tamasha la Sanaa la Sikukuu ya Mwezi la CMG kutangazwa moja kwa moja nje ya nchi
2021-09-20 08:47:06| CRI

Tamasha la Sanaa la Sikukuu ya Mwezi la CMG kutangazwa moja kwa moja nje ya nchi_fororder_微信图片_20210920094420

Tamasha la Sanaa la Sikukuu ya Mwezi la Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) litafanyika kesho Septemba 21 saa mbili usiku kwa saa za Beijing, na litatangazwa moja kwa moja kote duniani, ikiwa ni mara ya kwanza kwa tamasha hilo kutangazwa moja kwa moja nje ya nchi.

Televisheni ya Sinovison ya Marekani, Xinflix Media ya Canada, Switch TV ya Kenya, CATV ya Falme za Kiarabu na Enjoy TV ya Indonesia zinatarajiwa kutangaza tamasha hilo moja kwa moja. Aidha, CMG pia itatangaza tamasha hilo kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook na Youtube.