Jumuiya ya wahitimu waliosoma China yazinduliwa ili kuimarisha uhusiano kati ya Sudan kusini na China
2021-09-20 08:46:18| CRI

Jumuiya ya wahitimu waliosoma China ilizinduliwa ili kuimarisha uhusiano mzuri kati ya Sudan Kusini na China.

Akiongea kwenye hafla ya uzinduzi iliyofanyika Jumapili mjini Juba, Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya China katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan Kusini Bw. Simon Juach Deng, amesema Jumuiya ya Wahitimu waliosoma China ya Sudan Kusini (SSCAA) ni kilele cha uhusiano imara kati ya pande hizo mbili.

Bw. Deng amesema serikali ya China imeiunga mkono Sudan Kusini katika kuanzisha taasisi na miundombinu muhimu kwa ajili ya maendeleo yake. Ameihimiza jumuiya hiyo yenye wanachama zaidi ya 200, kutumia ujuzi na stadi walizopata kutokana na masomo yao katika vyuo vikuu mbalimbali vya China, kuinufaisha Sudan Kusini.