Chanjo ya COVID-19 iliyotolewa na China yawasili Burkina Faso
2021-09-20 09:24:11| cri

Chanjo ya COVID-19 iliyotolewa na China imewasili Ouagadougou nchini Burkina Faso. Balozi wa China nchini humo Li Jian, maofisa wa wizara ya mambo ya nje ya Burkina Faso na mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) wamehudhuria sherehe ya kupokea chanjo hiyo.

Balozi Li Jian amesema kuna jumla ya dozi laki 4 za Sinopharm zilizotolewa na China kwa Burkina Faso, ambayo ni ishara ya uhusiano mzuri kati ya nchi hizo mbili. Na anatarajia kuwa chanjo hiyo itaisaidia Burkina Faso kupambana na virusi vya Corona na kutunza afya ya raia wake.

Ofisa mwandamizi wa wizara ya mambo ya nje ya Burkina Faso    amesema sasa hali ya janga la virusi vya Corona inadhibitika nchini humo kutokana na msaada wa China. Amesema nchi yake itatumia vizuri chanjo hiyo kuwakinga raia wake na kupunguza maambukizi ya virusi vya Corona.

Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Burkina Faso Alimata Diarra-Nama amesema chanjo hiyo iliyotolewa na China imeidhinishwa na WHO, na usalama na ufanisi wake umetambuliwa na pande mbalimbali ambazo zimetoa chaguo jipya kwa raia wa nchi hiyo waliopokea chanjo.