Watu watano wajeruhiwa kwenye mlipuko wa mabomu yaliyotegwa ardhini katikati ya Somalia
2021-09-20 09:42:56| CRI

Mkuu wa wilaya ya Bulaburte ya Somalia Bw. Ahmed Mahad Nur amesema watu zaidi ya watano wamejeruhiwa katika mlipuko wa mabomu yaliyotegwa ardhini uliotokea katika uwanja wa ndege ulioko kwenye mkoa wa Hira katikati ya nchi hiyo.

Bw. Nur amesema wapiganaji wa kundi la Al-Shabaab waliingia kisiri katika uwanja huo uliojengwa upya na kutega mabomu ardhini yaliyolipuka baadaye.

Pia amesema, sehemu ya uwanja huo unaopangwa kuzinduliwa baadaye kufuatia kukamilika kwa kazi imeharibiwa kwa mabomu hayo.