Ujumbe wa AU kuitembelea Zambia
2021-09-21 09:40:39| CRI

Msemaji wa ubalozi wa Zambia nchini Ethiopia amesema ujumbe kutoka Umoja wa Afrika utaitembelea Zambia wiki hii na kufanya mikutano kuhusu jinsi ya kushirikiana na serikali ya Zambia kwenye kuharakisha na kudumisha ukuaji shirikishi barani Afrika.

Katibu wa kwanza wa habari na utalii wa Zambia Bw. Inutu Mupanga Mwansa alisema ujumbe huo utakaoongozwa na kamishna wa maendeleo ya uchumi, biashara, viwanda wa Umoja wa Afrika utawasili nchini Zambia Jumanne na kufanya mikutano mfululizo na maofisa waandamizi wa serikali. Watajadili jinsi mashirika ya bara la Afrika yatakavyoshirikiana na Zambia katika kuharakisha na kudumisha umoja wa Afrika ili kutimiza Ajenda ya AU ya mwaka 2083 kuhusu “Afrika Tunayotaka".