Tamasha la 11 la kimataifa la filamu lafunguliwa Beijing
2021-09-21 14:36:16| cri

Tamasha la 11 la kimataifa la filamu lafunguliwa Beijing_fororder_微信图片_20210921143212

Tamasha la 11 la kimataifa la filamu la Beijing lililoandaliwa na Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) na serikali ya mji wa Beijing limefunguliwa leo hapa Beijing.

Kwenye tamasha hilo, karibu filamu 300 kutoka nchi mbalimbali zitaoneshwa. Mashindano ya “Tuzo ya Tiantan” ya tamasha hilo yameshirikisha filamu 889 kutoka nchi 77 duniani, na hadi sasa filamu 15 zimeingia fainali.