UM kuunga mkono maendeleo ya mji wa kisasa wa Kenya
2021-09-21 09:28:34| CRI

Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP limesema, litaunga mkono Kenya kuendeleza mji wa kiteknolojia wa Konza.

Mjumbe wa shirika hilo nchini Kenya Bw. Walid Badawi amesema, shirika hilo litahimiza mji huo wa kisasa kujifunza kutoka kwa uzoefu wa kimataifa kutoka miji mingine ya kiteknolojia kote duniani.

Bw. Badawi amesema tutatoa uungaji mkono katika utekelezaji wa mpango wa kimkakati wa maendeleo ya mji wa Konza, huku akieleza kuwa watashirikiana na mji huo wa Kenya kuvutia wawekezaji na wavumbuzi kuanzisha shughuli zao.

Mji wa Konza ni mji wa kiteknolojia ulioko umbali wa kilomita 60 kutoka mji mkuu Nairobi. Mwaka 2013 Kenya ilipitisha mpango mkuu wa maendeleo ya mji wa kisasa huko Konza.