Serikali ya Rwanda yamhukumu Rusesabagina kifungo cha miaka 25
2021-09-21 09:03:06| CRI

Mahakama kuu ya Rwanda kitengo cha kimataifa na makosa ya kuvuka mpaka imemhukumu Bw. Paul Rusesabagina kifungo cha miaka 25 gerezani baada ya kumkuta na hatia ya tuhuma za ugaidi.

Bw. Rusesabagina aliyepata umaarufu baada ya kuigizwa kwenye filamu ya Hotel Rwanda na filamu hiyo kupata tuzo ya Oscar, hakuwepo mahakamani wakati akihukumiwa.

Amekutwa na hatia ya kuwa sehemu ya kundi linalofanya mashambulizi dhidi ya Rwanda, kuua raia, kuwajeruhi na kupora mali zao. Kwenye hukumu ya mwisho jaji Antoine Muhima amesema Bw. Rusesabagina ana hatia ya kuunda kundi la kigaidi na kufanya mashambulizi ya kigaidi nchini Rwanda.

Mbali na Rusesabagina, aliyekuwa kamanda na msemaji wa kundi la FNL Bw. Callixte Nsabimana pia alihukumiwa kifungo cha miaka 20 na mahakama hiyo kwa kosa la kukanusha mauaji ya kimbari ya mwaka 1994.