Zimbabwe yashirikiana na kampuni ya Huawei kuboresha miundombinu ya Tehama
2021-09-21 09:03:53| CRI

Rais Emmerson Mnangagwa jana alizindua mradi wenye lengo la kupanua huduma na miundombinu ya Tehama nchini Zimbabwe.

Mradi huo ambao kwa sasa uko kwenye awamu ya tatu inatekelezwa kwa ushirikiano na kampuni ya Huawei ya China na kampuni ya pili kwa ukubwa ya mawasiliano ya simu ya Zimbabwe NetOne.

Mradi huo unaogharamiwa na benki ya Exim ya China utagharimu dola za kimarekani milioni 71, na ni mradi wa ushirikiano wa kimkakati kati ya serikali za China na Zimbabwe, wenye lengo la kufikisha huduma ya internet kwa simu za mkononi katika maeneo ya mbali nchini Zimbabwe.

Awamu ya kwanza ya mradi huo ilianza mwaka 2011 na kukamilika mwaka 2013 na kuweka vituo 100 vya huduma ya 3G na 350 vya huduma ya 2G. Awamu ya pili ilianza mwaka 2014 na kuongeza vituo 2,231.