China yaandaa mashindano ya picha nchini Somalia ili kuimarisha uhusiano wa nchi mbili
2021-09-21 09:07:20| CRI

Ubalozi wa China nchini Somalia umesema utaandaa Mashindano ya Picha ya Urafiki kati ya China na Somalia ili kusaidia kuimarisha uhusiano kati ya pande mbili kabla ya maadhimisho ya miaka 72 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China.

Ubalozi huo umesema mashindano hayo yatasherehekea urafiki wa kina kati ya China na Somalia, na kuimarisha mawasiliano kati ya watu wa nchi hizo mbili.

Kwa mujibu wa ubalozi huo washiriki wa mashindano hayo wanatarajiwa kuwasilisha picha zao kuanzia Septemba 20 hadi 26 kuhusu ushirikiano kati ya China na Somalia kwenye nyanja mbalimbali, na urafiki na mawasiliano kati ya watu wa nchi hizo mbili. Matokeo ya mashindano hayo yatatangazwa mtandaoni Septemba 28, na zawadi zitatolewa kwa washindi kabla ya Oktoba 31.