Zanzibar yawaalika wawekezaji kushiriki kwenye ukarabati wa maeneo ya kihistoria
2021-09-21 09:20:57| cri

Mamlaka ya Zanzibar, Tanzania imetangaza Jumatatu wiki hii kuwa itawaalika wawekezaji wenyeji na wa nje kuwekeza kwenye maendeleo na ukarabati wa maeneo ya kihistoria huko Zanzibar.

Waziri wa Utalii na Urithi wa Zanzibar Lela Mohamed Mussa, amesema maeneo yanayohitaji kukarabatiwa ni pamoja na majengo ya mji kongwe ambao umetambuliwa kwenye Orodha ya Urithi wa Dunia ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO.