AU: Waafrika wengi wana wasiwasi juu ya chanjo ya COVID-19 kutokana na taarifa potofu
2021-09-22 08:40:02| CRI

Umoja wa Afrika umesema kusambaa kwa taarifa potofu kuhusu chanjo ya COVID-19 kunawafanya watu wengi barani Afrika wawe na wasiwasi juu ya kudungwa chanjo hiyo.

Mkurugenzi wa Sekretarieti ya Baraza la Uchumi, Jamii na Utamaduni la Umoja wa Afrika Bw. William Carew amewahimiza waafrika kujitokeza kupata chanjo ili kutimiza kinga ya jamii, na hivi sasa ni asilimia 3.6 tu ya watu wa Afrika ndio wamepata dozi kamili za chanjo ya COVID-19.

Bw. Carew ametoa wito kwa waafrika kufuata pendekezo la wataalamu wa afya ya umma kuwa chanjo bado ni njia pekee inayotekelezeka ya kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona. Pia ameyataka mashirika ya taasisi zisizo za kiserikali ya Afrika kueneza taarifa sahihi kuhusu chanjo ili kuelimisha jamii wanazozifanyia kazi.