Rais Xi Jinping atoa salamu kwa wakulima kabla ya sikukuu ya mavuno
2021-09-23 09:28:58| CRI

Rais Xi Jinping atoa salamu kwa wakulima kabla ya sikukuu ya mavuno_fororder_VCG111256583173

Rais Xi Jinping wa China ametoa salamu kwa wakulima na watu wengine wanaoshughulikia mambo ya kilimo na vijiji kabla ya sikukuu ya nne ya mavuno ya wakulima ya China.

Rais Xi ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China, amesisitiza kuwa inapaswa kuharakisha juhudi za kuendeleza mambo ya kilimo na vijiji kuwa ya kisasa, na kuboresha maisha ya wakulima.

Amesema mwaka huu China imeshinda janga la COVID-19 na maafa ya asili, na kuhakikisha mavuno ya nafaka na uzalishaji wa kilimo, hali ambayo imechangia juhudi za kupata maendeleo mapya wakati wa mabadiliko, na kudumisha utulivu wa jumla.