Mwenyekiti wa baraza la utawala la Sudan amesema jeshi halina nia ya kutwaa madaraka
2021-09-23 08:39:55| CRI

Mwenyekiti wa baraza la utawala la Sudan amesema jeshi halina nia ya kutwaa madaraka_fororder_src=http___www.xinhuanet.com_photo_2021-09_21_1127886292_16322291896661n&refer=http___www.xinhuanet

Mwenyekiti wa Baraza la Utawala nchini Sudan Abdel Fattah Al-Burhan amekanusha madai kuwa kuna nia ya jeshi la Sudan kutwaa madaraka, kufuatia jaribio la mapinduzi lililofanywa jumanne na maofisa kadhaa wa jeshi la nchi hiyo.

Kwenye hotuba aliyoitoa katika Kambi ya Jeshi ya Al-Markhiyat, kaskazini mwa mji mkuu Khartoum,  Bw. Al-Burhan amesema vikosi vya jeshi la Sudan ndivyo vilivyozuia jaribio la mapinduzi. Amesema wana uhakika na mabadiliko ya kidemokrasia, na jeshi halina nia ya kutwaa madaraka.

Hata hivyo amelaani makundi mbalimbali ya kisiasa, ambayo amesema hakuna kundi lolote linalozungumzia uchaguzi au kumalizika kwa kipindi cha mpito, wanachojali ni kuendelea kuwa madarakani.

Mapema kabla ya hotuba ya Bw. Al-Burhan, waziri Mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok alisema jaribio la mapinduzi lilipangwa na watu wa ndani na nje ya jeshi.