Balozi wa China: Mabadiliko ya tabianchi yahitaji mwitikio wa dunia nzima
2021-09-24 10:08:26| CRI

Balozi wa China: Mabadiliko ya tabianchi yahitaji mwitikio wa dunia nzima_fororder_张军

Balozi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Zhang Jun amesema, mabadiliko ya tabianchi ni changamoto inayowakabili binadamu wote, na inahitaji mwitikio wa dunia nzima.

Balozi Zhang amesisitiza kuwa ni muhimu kwa nchi zilizoendelea kutimiza kihalisi majukumu na ahadi zao katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, kwani zina wajibu wa kihistoria katika suala hilo.

Amesema badala ya kuzikazia macho nchi nyingine kila wakati, nchi zilizoendelea zinapaswa kuchukua hatua madhubuti ili kupunguza utoaji wa hewa zinazoongeza joto, na kutatua mapema iwezekanavyo pengo la dola bilioni 100 za kimarekani ambazo zingetoa kabla ya mwaka 2020.