Misri kuzindua mstari wa pili wa kuzalisha chanjo ya Sinovac ndani ya wiki tano
2021-09-24 08:37:36| CRI

Misri kuzindua mstari wa pili wa kuzalisha chanjo ya Sinovac ndani ya wiki tano_fororder_VCG111327703349

Waziri wa Afya wa Misri Hala Zayed amesema Misri itazindua mstari wa pili wa kuzalisha chanjo ya Sinovac ya China dhidi ya COVID-19 ndani ya wiki tano zijazo.

Chanjo hiyo inazalishwa na shirika la taifa la chanjo nchini Misri Vacsera, kwenye eneo la Agouza mkoani Giza karibu na mji mkuu Cairo.

Akiongea kwenye mkutano na wanahabari akiwa pamoja na balozi wa Ujerumani nchini Misri Frank Hartmann, Bw. Zayed amesema wameshapata malighafi za kuzalisha dozi milioni 15 za chanjo hiyo, na sasa wanapokea shehena nyingine kwa ajili ya kuzalisha dozi nyingine milioni 15.

Julai 18, waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi ambaye alikuwa ziarani nchini Misri na mwenzake wa Misri Sameh Shoukry walihudhuria hafla ya uzalishaji wa pamoja wa dozi milioni 1 za chanjo ya Sinovac nchini humo, ikiwa ni nchi ya kwanza barani Afrika kushirikiana na China kwenye uzalishaji wa chanjo ya COVID-19.