China yatoa dozi bilioni 1.2 za chanjo ya COVID-19 na malighafi za chanjo kwa nchi na mashirika ya nje
2021-09-24 09:24:30| CRI

China yatoa dozi bilioni 1.2 za chanjo ya COVID-19 na malighafi za chanjo kwa nchi na mashirika ya kimataifa zaidi 100_fororder_VCG111347766325

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Zhao Lijian amesema hadi sasa China imetoa dozi bilioni 1.2 za chanjo na malighafi za chanjo kwa nchi na mashirika ya kimataifa zaidi ya 100, na kutoa msaada wa vifaa kwa nchi zaidi ya 150 na mashirika 14 ya kimataifa kwa ajili ya kupambana na janga.

Katika mjadala wa kikao cha 76 cha baraza kuu la Umoja wa Mataifa, Rais Xi Jinping alisema kuifanya chanjo ya COVID-19 kama bidhaa ya umma duniani, kuhakikisha upatikanaji wa chanjo kwa nchi zinazoendelea, ni muhimu kwamba chanjo zisambazwe kwa usawa duniani.

Bw. Zhao Lijian amesisitiza China itaendelea kushirikiana na nchi mbalimbali katika mapambano dhidi ya janga hilo na kutoa mchango kwa ufufuaji wa uchumi duniani.