Shirika la AU lasema utawala bora barani Afrika unazidi kuboreka
2021-09-24 09:03:37| CRI

Shirika maalum la Umoja wa Afrika (AU), la mfumo wa mapitio ya utawala (APRM), limesema utawala bora kwenye serikali za kitaifa barani Afrika umekuwa ukiongezeka.

Mkurugenzi Mtendaji wa APRM Bw. Eddy Maloka, ameuambia Umoja wa Afrika huko Nairobi kwamba kumekuwa na ongezeko la kuheshimu utawala kwa mujibu wa sheria, na mwamko mkubwa wa kutumia taratibu za kikatiba katika kuondoa tofauti.

Hata hivyo amehimiza kuboreshwa zaidi kwa kiwango cha utawala bora, kwa sababu hatua hiyo itachochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika bara la Afrika.

Amesema Afrika ni bara pekee lenye utaratibu wa kufanya mapitio ya utendaji wa nchi kuhusu utawala bora, demokrasia, haki za binadamu, usimamizi wa uchumi, usimamizi wa makampuni na maendeleo ya kijamii na kiuchumi.