Maonyesho ya pili ya Uchumi na Biashara ya China-Afrika kufanyika mjini Changsha, China
2021-09-26 10:18:15| cri

Maonyesho ya pili ya Uchumi na Biashara ya China-Afrika kufanyika mjini Changsha, China_fororder___172.100.100.3_temp_9500049_1_9500049_1_1_26ad5e43-22d5-4d45-866b-b3fbf9ae5e5f

Maonyesho ya pili ya Uchumi na Biashara ya China-Afrika kufanyika mjini Changsha, China_fororder___172.100.100.3_temp_9500049_1_9500049_1_1_1f128eae-8186-4549-b790-a86a236164e1

Maonyesho ya pili ya Uchumi na Biashara ya China-Afrika kufanyika mjini Changsha, China_fororder___172.100.100.3_temp_9500049_1_9500049_1_1_3db9573a-d60a-4bd1-a5c1-094cc5b73c3d

Maonyesho ya awamu ya pili ya Uchumi na Biashara ya China-Afrika yatafanyika kuanzia tarehe 26 hadi tarehe 29 mwezi huu huko mji wa Changsha, mkoani Hunan nchini China.

Kwa ujumla makampuni karibu 900 kutoka China na Afrika zimejiandikishwa kushiriki kwenye maoneysho hayo. Kati yao, kuna makampuni na mashirika kutoka nchi karibu 40 za Afrika zikiwemo Uganda, Tanzania, Mali na Ghana, ambapo nchi sita za Afrika yaani Algeria, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Afrika Kusini, Senegal zimekuwa nchi wageni waalikwa katika maonyesho hayo.

Katika jumba kuu la maoneysho hayo lenye eneo la mita za mraba elfu 64, pia yatafanyika maoneysho ya mafanikio ya ushirikiano wa biashara na uchumi kati ya China na Afrika na maonyesho ya bidhaa kutoka Afrika, ambayo yanatarajiwa kutoa nafasi kubwa zaidi kwa bidhaa kutoka Afrika kuonyeshwa kwenye soko la China.