Awamu ya nne ya msaada wa chanjo ya COVID-19 uliotolewa na China yawasili Zimbabwe
2021-09-27 08:43:45| cri

Makamu wa Rais wa Zimbabwe ambaye pia ni Waziri wa Afya Bw. Constantino Chiwenga, jana mjini Harare, alipokea awamu ya nne ya msaada wa chanjo ya COVID-19 uliotolewa na China kwa Zimbabwe.

Bw. Chiwenga ameishukuru China kwa kutoa msaada huo wa chanjo kwa Zimbabwe na kuisaidia nchini hiyo kuwa moja ya nchi zilizo na kiwango cha juu cha utoaji wa chanjo ya COVID-19 barani Afrika.

Kwa upande wake, balozi wa China nchini Zimbabwe Bw. Guo Shaochun amesema, China na Zimbabwe zimepata mafanikio mazuri katika kupambana na janga hilo. Katika siku zijazo, nchi hizo mbili zitaendelea kushirikiana ili kuimarisha ushirikiano katika nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na dawa na afya, na kusukuma mbele uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati yao ufikie ngazi ya juu zaidi.