Tanzania yanunua chanjo za Corona kutoka China
2021-09-27 14:27:10| cri

Msemaji wa serikali ya Tanzania Bw. Gerson Msigwa jana alitangaza kuwa serikali ya Tanzania imenunua chanjo za Corona milioni mbili kutoka China, ili kukidhi mahitaji ya mpango wa sasa wa kutoa chanjo.

Akizungumza na wanahabari Bw. Msigwa amesema kwa sasa, Tanzania imeingia katika awamu ya pili ya kutoa chanjo za Corona, lakini wananchi bado hawana hamu ya kutosha ya kupata chanjo. Ili kuongeza kiwango cha kupata chanjo, serikali ya Tanzania imeongeza idadi ya vituo vya kutoa chanjo kutoka 550 vya awamu ya kwanza hadi 5,784. Zaidi ya hayo, watumishi wa afya kutoka baadhi ya sehemu za nchi hiyo watafanya kazi ya kuwaelimisha watu katika kupata chanjo ili kuongeza kiwango cha kupata chanjo kwenye sehemu za vijijini.