Sudan yasema mvutano uliopo sasa nchini humo sio kati ya jeshi na wananchi
2021-09-27 08:49:20| CRI

Sudan yasema mvutano uliopo sasa nchini humo sio kati ya jeshi na wananchi_fororder_苏丹总理哈姆杜克

Waziri mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok amesema, mvutano uliopo sasa nchini humo sio kati ya jeshi na raia, bali ni kati ya wale wanaounga mkno mageuzi ya kidemokrasia ya kiraia na wale wanaotaka kuzuia hatua hiyo.

Katika hotuba yake aliyoitoa jana kupitia televisheni nchini humo, Bw. Hamdok amezitaka pande zote husika kufuata kithabiti waraka wa kikatiba, kujizuia kuchukua msimamo wa upande mmoja, na kubeba kikamilifu majukumu yao.

Mapema jana, vikosi vya usalama vilijitoa katika ulinzi wa makao makuu ya kamati ya uwezeshaji wa utenguzi wakati mvutano ukiongezeka kati ya upande wa jeshi na raia katika serikali ya mpito nchini Sudan.