Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa atoa wito wa kuondoa silaha za nyuklia
2021-09-27 08:50:21| CRI

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa atoa wito wa kuondoa silaha za nyuklia_fororder_timg (5)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema silaha zote za nyuklia zinapaswa kuondolewa duniani na ni lazima zama mpya ya majadiliano, uaminifu na amani ianze.

Akizungumza katika Siku ya Kimataifa ya Kuondoa Silaha za Nyuklia iliyoadhimishwa jana Jumapili, Guterres amesema tishio la silaha za nyuklia limekuwa kazi kuu ya Umoja wa Mataifa tangu ulipoanzishwa.

Amesema ingawa idadi kamili ya silaha za nyuklia imekuwa ikipungua kwa miongo kadhaa, lakini karibu silaha 14,000 za nyuklia zimehifadhiwa, jambo ambalo ni tishio kubwa la nyuklia kwa karibu miongo minne.

Guterres ameongeza kuwa, huu ni wakati wa kuondoa wingu hili kikamilifu, kuharibu silaha za nyuklia katika dunia, na kuingiza zama mpya ya majadiliano, uaminifu na amani kwa watu wote.