Raia 12 wauawa katika mapambano kati ya wanajeshi na wapiganaji nchini DRC
2021-09-28 08:50:31| CRI

 

 

Raia 12 wameuawa katika mapambano makali kati ya vikosi vya jeshi la serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Kundi la The Patriotic Force and Integrationist of Congo (FPIC) yaliyotokea Jumapili usiku mjini Makayanga, kaskazini mashariki mwa mkoa wa Ituri.

Msemaji wa jeshi katika mkoa huo Luteni Jules Ngongo amesema, wapiganaji wanane waliuawa wakati wa mapigano hayo, na kuongeza kuwa mji ulioathirika uko chini ya udhibiti wa vikosi vya jeshi.

Kundi la FPIC lilianzishwa mapema mwaka huu na wakazi wa eneo hilo ili kupambana na waasi wa Kundi la Allied Democratic Forces (ADF) linalofanya mashambulizi mara kwa mara katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Ituri.