Shirikisho la Urafiki kati ya China na Misri wapongeza uhusiano wa muda mrefu kati ya nchi hizo
2021-09-28 08:53:45| CRI

Shirikisho la Urafiki kati ya China na Misri wapongeza uhusiano wa muda mrefu kati ya nchi hizo_fororder_unnamed

Shirikisho la Urafiki kati ya Misri na China limepongeza uhusiano wa muda mrefu wa kirafiki na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

Akizungumza katika semina iliyowakutanisha wanadiplomasia, wafanyabiashara, wataalamu na waandishi wa China na Misri katika kusherehekea miaka 72 ya kuasisiwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, mwenyekiti wa Shirikisho hilo Ahmed Waly amesema, miongo michache baada kuanzishwa kwa Jamhuri hiyo, China inaongoza katika sekta za uchumi, sayansi na teknolojia, na kufanikiwa kuondokana na umasikini uliokithiri.

Kwa upande wake, Balozi wa China nchini Misri Liao Liqiang amesema, mwaka huu ni wa 65 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Misri, na kwamba nchi hizo zimeshirikiana katika shida na raha, hususan baada ya mlipuko wa virusi vya Corona, ambapo ziliimarisha zaidi ushirikiano wao katika kupambana na janga hilo kwa pamoja.

Ameongeza kuwa, thamani ya biashara kati ya nchi hizo imefikia dola za kimarekani bilioni 14.53 mwaka jana, ikiwa ni ongezeko la asilimia 10.1 ikilinganishwa na mwaka 2019.