Wazimbabwe waaswa kutokubali kutumiwa na Marekani dhidi ya China
2021-09-28 15:37:45| Cri

Gazeti la The Herald la Zimbabwe limetoa tahariri likisema kuwa Marekani na baadhi ya nchi za Magharibi zimejikita katika kudhamini vyombo vya habari, vyama vya wafanyakazi, asasi za kiraia na mawakili ili kupambana na uwekezaji wa China nchini Zimbabwe.

Inaonekana kwamba Marekani inahisi joto la kupaa kwa China, ambayo sasa ni nchi ya pili kwa uchumi mkubwa duniani na inakwenda sambamba na nchi hiyo iliyokuwa na nguvu pekee kubwa duniani.

Tahariri hiyo imeendelea kusema kuwa madai mengi ya uongo yametolewa dhidi ya taifa na makampuni ya China bila ya kujaribu kuthibitisha ukweli yakiwa na lengo la kuchochea uhasama kati ya China na Zimbabwe. Cha kusikitisha zaidi ni kwamba baadhi ya Wazimbabwe wanakubali kutumiwa na Marekani dhidi ya China kwa kupewa bahashishi ndogo tu labda dola za kimarekani 1000. Hivyo tahariri hiyo imewasihi Wazimbabwe kuona ni nani rafiki yao na nani adui yao na pia wanatakiwa kutambua kuwa haki na usawa havilipwi kwa pesa.