Watu 34 wauawa katika shambulizi lililofanywa na watu wenye silaha kaskazini magharibi mwa Nigeria
2021-09-28 08:54:25| CRI

Watu 34 wauawa katika shambulizi lililofanywa na watu wenye silaha kaskazini magharibi mwa Nigeria_fororder_webwxgetmsgimg (2)

Watu 34 wameuawa na wengine 7 kujeruhiwa kwenye shambulizi lililofanywa na watu wenye silaha wasiojulikana katika mkoa wa Kaduna, kaskazini magharibi mwa Nigeria.

Kamishna wa usalama wa ndani na masuala ya familia nchini humo Samuel Aruwan amesema, vyombo vya usalama vimeripoti mauaji hayo yaliyotokea usiku wa jumapili kwenye kijiji cha Madamai, eneo la Kaura katika mkoa huo.

Amesema askari saba walijeruhiwa na baadhi ya nyumba kuchomwa moto wakati wa shambulizi hilo, na kuongeza kuwa washukiwa wawili wanahojiwa kwa tuhuma za kuhusika na shambulizi hilo.