Ripoti: Tanzania ni miongoni mwa maeneo kumi makubwa ya uwekezaji katika Afrika
2021-09-29 10:45:11| cri

Tanzania ni miongoni mwa maeneo kumi makubwa ya uwekezaji katika Afrika, kutokana na mageuzi na mazingira mazuri ya uwekezaji yaliyowekwa na serikali.

Kwa mujibu wa ripoti ya “Wapi pa kuwekeza katika Afrika mwaka 2021” iliyotolewa hivi karibuni, Benki ya RMB imeshika nafasi ya kumi kwa vivutio vya uwekezaji. Tanzania imekuwa kwenye kasi ya mendeleo katika miaka michache iliyopita, kasi ambayo pia imeshuhudiwa kama moja ya nchi zenye uchumi unaokua kwa kasi zaidi barani Afrika ikichukua nafasi ya tatu ndani ya EAC.

Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa hivi karibuni alibainisha kuwa idadi ya miradi mipya ya uwekezaji iliyosajiliwa Tanzania kati ya Machi na Agosti mwaka 2021, imeongezeka hadi 133, ikiwa na thamani ya dola za kimarekani bilioni 2.98.