Watu watano wauawa katika shambulizi dhidi ya msafara wa wachimbaji madini magharibi mwa Mali
2021-09-29 08:54:46| cri

Jeshi la Mali limesema, watu watano wameuawa na wengine wanne kujeruhiwa katika shambulizi dhidi ya msafara wa wachimbaji wa madini uliokuwa ukilindwa na jeshi hilo karibu na mji wa Kolokani, magharibi mwa nchi hiyo.

Mpaka sasa, hakuna kundi lolote lililodai kuhusika na shambulizi hilo.