Kenya yatoa wito wa kuongeza juhudi katika mapambano dhidi ya Malaria
2021-09-29 09:09:53| cri

Kenya yatoa wito wa kuongeza juhudi katika mapambano dhidi ya Malaria_fororder_VCG111167229737

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya malaria, licha ya janga linaloendelea sasa la virusi vya Corona.

Akizungumza kwa njia ya video katika Baraza la Kumaliza Malaria (EMC) mjini Nairobi, rais Kenyatta amesema, kutokana na nguvu zaidi kuelekezwa katika mapambano dhidi ya virusi vya Corona, majanga mengine kama malaria ambayo yanasababisha vifo vya watu wengi barani Afrika yamesahaulika.

Rais Kenyatta, ambaye pia ni mwenyekiti wa zamu wa Muungano wa Viongozi wa Afrika wa Kudhibiti Malaria (ALMA), amesisitiza kusimamia ajenda nne za Muungano huo, huku ajenda muhimu zaidi kati ya hizo ikiwa ni kuboresha teknolojia za kidijitali na matumizi ya data halisi ikiwemo kubadilishana taarifa za mafanikio katika kupambana na malaria kati ya nchi wanachama. Amesema hatua hiyo inaweza kutumika katika kupambana na majanga yaliyoko sasa na yanayoweza kutokea siku zijazo.