Korea Kaskazini yafanya majaribio ya kurusha kombora jipya
2021-09-29 10:43:08| cri

Shirika la Habari la Korea Kaskazini leo limeripoti kuwa Korea Kaskazini jana asubuhi ilifanya majaribio ya kurusha kombora lenye kasi la Hwasong-8 huko Toyang-ri wilayani Ryongrim mkoani Jagang.

Ripoti imesema kombora hilo jipya lilitengenezwa na kufanyiwa majaribio na chuo cha sayansi ya ulinzi cha nchi hiyo. Kwenye majaribio ya kwanza, wanasayansi wa ulinzi wa taifa walithibitisha kazi ya udhibiti na utulivu wa kombora hilo, pamoja na sifa mbalimbali za kombora. Jaribio hilo limethibitisha kuwa vipimo kamili vya teknolojia vinaendana na vigezo vya mpango.