Malengo ya “Mpango wa Utekelezaji wa Haki za Binadamu wa Taifa wa China (mwaka 2016 hadi mwaka 2020)” yote yakamilika
2021-09-29 15:19:15| Cri

Ripoti ya tathmini ya utekelezaji wa “Mpango wa Utekelezaji wa Haki za Binadamu wa Taifa wa China kuanzia mwaka 2016 hadi mwaka 2020” iliyotolewa leo imesema malengo na majukumu yaliyowekwa katika Mpango huo yote yamekamilika, ambapo viashiria na majukumu mengi yalitekelezwa kabla ya mpango au kwa kiwango cha kuzidi mpango.

Ripoti hiyo imesema, mwezi Septemba mwaka 2016, serikali ya China ilitangaza Mpango huo. Hii ilikuwa ni awamu ya tatu kwa China kutunga mpango wa kitaifa kuhusu haki za binadamu na kuamua malengo na majukumu ya kuheshimu, kulinda na kuhimiza haki za binadamu kitaifa katika kipindi cha kuanzia mwaka 2016 hadi mwaka 2020.

Ripoti hiyo inasema kwa ujumla, katika kipindi hicho, serikali ya China imeshikilia kuyapa kipaumbile maendeleo ya wananchi, kutekeleza kanuni ya “kuheshimu na kulinda haki za binadamu” kwa mujibu wa katiba, na kuchukua hatua halisi kutekeleza malengo na majukumu yote yaliyowekwa katika Mpango huo wa utekelezaji. Cha kusisitizwa ni kuwa katika kipindi hicho, China imekamilisha majukumu ya kutokomeza kabisa umaskini uliokithiri, kujenga jamii yenye maisha bora, kiwango cha kulinda haki za binadamu kwa watu wa China kimeboreshwa, na hisia za watu kuhusu kumiliki, kufurahia na usalama zimeongezeka.

Hata hivyo, ripoti hiyo imekiri kuwa China ikiwa nchi kubwa inayoendelea, kazi ya kuboresha haki za binadamu bado haijakamilika, na inahitajika kuendelea kufanywa.