Mashirika ya ndege ya Afrika Kusini na Kenya yashirikiana katika kuboresha huduma
2021-09-29 10:43:48| cri

Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA) limetia saini Mkataba wa Ushirikiano (MoC) na Shirika la Ndege la Kenya ili kukuza uwezo wa ukuaji wa pande hizo mbili kwa kutumia nguvu za vituo vya mashirika hayo mawili ya ndege vye shughuli nyingi.

Kwa mujibu wa MoC, mashirika hayo mawili ya ndege yatashirikiana katika nyanja za uchumi, ufundi, matengenezo na ukarabati, na kutumia fursa kupata kiwango kikubwa cha uchumi.

SAA ilisema hii itasaidia katika usanifishaji wa bidhaa na utoaji wa huduma unaolingana na mwenendo wa sasa wa safari za anga.

Mkurugenzi Mtendaji wa muda wa SAA Bw. Thomas Kgokolo amesema kuwa pamoja na kuwa shirika mwenyeji lenye nguvu, sehemu ya mkakati wa ukuaji wake ni kushirikiana na shirika la ndege la Kenya ambalo ni moja ya mashirika yenye nguvu na kuheshimika barani Afrika.