Umoja wa Mataifa wasema mgogoro wa kibinadamu mkoani Tigray, Ethiopia unakuwa mbaya zaidi
2021-09-30 08:53:56| CRI

Mratibu wa Misaada ya Dharura wa Umoja wa Mataifa, Martin Griffiths amesema, mgogoro wa kibinadamu katika mkoa wa Tigray nchini Ethiopia unaelekea katika hali mbaya zaidi, huku watu milioni 5.2 wakihitaji msaada wa chakula, na laki 4 kati yao wakiwa kwenye mazingira yanayokaribia ukame.

Amesema, nzige wa jangwani, mavuno hafifu, misaada ya kibinadamu kushindwa kufika mkoani humo, na mapigano yaliyofikia mikoa ya jirani ya Amhara na Afar kuwa mambo yanayochochea hali ya kibinadamu kuwa mbaya zaidi.

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema, Griffiths anaendelea kuwasiliana na mamlaka za serikali ya Ethiopia ili kuondoa vizuizi vya njiani na kuruhusu misafara ya misaada kuendelea kuingia mkoani humo.