DRC yapokea msaada wa chanjo za COVID-19 uliotolewa na China
2021-09-30 09:53:04| cri

 

 

Chanjo zilizotengenezwa na kampuni ya Sinovac zilitolewa na serikali ya China, zimewasili jana mjini Kinshasa, mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) .

Akizungumza kwenye hafla ya kupokea chanjo hizo, Waziri wa afya wa DRC Jean-Jacques Mbungani amesema, chanjo hizo zitaisaidia DRC katika mapambano dhidi ya COVID-19, na ameishukuru sana serikali ya China kwa msaada huo.

Mbungani amesisitiza kuwa, usalama na ufanisi wa chanjo za Sinovac umethibitishwa kikamilifu, na kuwataka raia wajitokeze na kupata dozi zote kamili za chanjo hiyo.