Maonesho ya Pili ya Uchumi na Biashara kati ya China na Afrika yasaini miradi 135 ya ushirikiano
2021-09-30 20:02:03| Cri

Msemaji wa Wizara ya biashara ya China Bibi Shu Jueting amesema Maonesho ya Pili ya Uchumi na Biashara kati ya China na Afrika yamepata mafanikio mazuri.

Shu amesema hayo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo hapa Beijing.

Kwenye mkutano huo Shu ameeleza kuwa maonesho hayo yanafuata umaalumu na mwelekeo mpya wa ushirikiano wa uchumi na biashara kati ya China na Afrika, kuandaa shughuli mbalimbali zikiwemo makongamano ya vyakula na bidhaa za kilimo, matibabu, madawa na afya, miundo mbinu na ushirikiano wa minyororo ya viwanda, kusaini nyaraka za ushirikiano za miradi 135 kupitia mtandao wa Internet na nje ya mtandao, na thamani ya miradi hiyo imefikia dola za kimarekani bilioni 22.9.