Uchumi wa Kenya wakadiriwa kuongezeka kwa asilimia 6.1 katika mwaka 2021
2021-09-30 10:42:58| cri

Benki kuu ya Kenya jana ilisema uchumi wa Kenya unakadiriwa kuongezeka kwa asilimia 6.1 katika mwaka 2021 baada ya kupungua kwa asilimia 0.3 mwaka jana.

Gavana wa Benki kuu ya Kenya Bw. Patrick Njoroge amesema ufufukaji wa uchumi unaanza kuonekana kwenye sekta kadhaa, hasa kwenye sekta ya huduma kama vile hoteli, ambayo iliathiriwa vibaya na janga la Corona mwaka jana. Ameongeza kuwa sekta ya kilimo pia inapaswa kutiliwa maanani, kwani inaweza kuathiriwa kutokana na mvua. Sekta ya kilimo itakuwa nguvu kubwa ya kuhimiza ongezeko la uchumi kwa mwaka 2021, na unakadiriwa kukua kwa asilimia 2.6.

Takwimu kutoka benki hiyo zimeonyesha kuwa uchumi wa Kenya utakua kwa asilimia 5.6 katika mwaka 2022, ambao utakuwa ni mwaka wa uchaguzi wa rais unaohusiana na kasi ndogo ya ukuaji wa pato la taifa (GDP).