Ubalozi wa China nchini Rwanda wazindua chemsha bongo ya Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhusiano wa Kibalozi
2021-10-01 10:01:35| cri

Katika Maadhimisho ya miaka 50 ya kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Rwanda na China, ubalozi wa China nchini Rwanda umezindua shindano la chemsha bongo mtandaoni ambapo watu tofauti watapata fursa ya kuonyesha ujuzi wao kuhusu uhusiano kati ya nchi hizo mbili. Rwanda na China zilianzisha uhusiano wa kidiplomasia Novemba 12, 1971. Serikali zote mbili zinachukua maadhimisho ya miaka 50 ya kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati yao, kama fursa ya kupanga maendeleo ya uhusiano wa nchi hizo katika miaka 50 ijayo, na kufungua maeneo mapya ya ushirikiano.