Mwakilishi wa nchi 78 atoa wito wa kupambana na ubaguzi wa rangi
2021-10-01 10:02:11| cri

Kutokana na pendekezo la pamoja la China na nchi za Afrika, Nigeria inawakilisha nchi 78 kuhutubia mjadala wa Kamati ya Tatu ya Mkutano Mkuu wa 76 wa Umoja wa Mataifa, ikieleza wasiwasi mkubwa juu ya ubaguzi wa rangi, matumizi ya nguvu ya polisi, na kukoseka kwa usawa wa kijamii, na kutoa wito wa kuharakisha utekelezaji wa “Azimio la Durban na Mwongozo wa mpango wa utekelezaji”, kupambana na aina zote za ubaguzi wa rangi, na chuki dhidi ya wageni.

Hotuba hiyo pia inasisitiza kuwa, kila mtu anazaliwa na uhuru, heshima na haki, na ana uwezo wa kuchangia maendeleo ya kijamii na ustawi. Nadharia yoyote ya ubora wa rangi inapaswa kulaumiwa na kukataliwa, na si haki tena ni hatari kwa jamii.