Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ashangazwa na uamuzi wa Ethiopia wa kuwafukuza maofisa 7 wa Umoja huo
2021-10-01 09:36:29| CRI

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ashangazwa na uamuzi wa Ethiopia wa kuwafukuza maofisa 7 wa Umoja huo_fororder_古特雷斯

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameeleza kushangazwa na taarifa za serikali ya Ethiopia kuwatangaza maofisa saba wa Umoja huo, wakiwemo maofisa waandamizi wa masuala ya kibinadamu, kama watu wasiokubalika na kuwaamuru kuondoka nchini humo.

Katika taarifa yake, Guterres amesema operesheni zote za kibinadamu zinaongozwa na kanuni za msingi za ubinadamu, kutokuwa na upendeleo, usawa, na uhuru, na nchini Ethiopia, Umoja huo unatoa msaada wa kuokoa maisha, ikiwemo chakula, dawa, na mahitaji ya afya kwa watu wenye uhitaji.

Jana Alhamis, Wizara ya Mambo ya Nje ya Ethiopia ilitangaza maofisa saba wa Umoja wa Mataifa kuwa watu wasiokubalika kwa tuhuma za kuingilia mambo ya ndani ya nchi hiyo, na kuwapa saa 72 kuondoka nchini Ethiopia.