WHO yasema nchi 15 za Afrika zafikia asilimia 10 ya lengo la kutoa chanjo za COVID-19
2021-10-01 09:37:37| CRI

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema, nchi 15 za Afrika zimetoa chanjo kamili ya COVID-19 kwa asilimia 10 ya wananchi wao, na kutimiza lengo lililowekwa na Mkutano wa Afya wa Dunia uliofanyika mwezi Mei.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya WHO kanda ya Afrika imesema, Seychelles na Mauritius zimetoa chanjo hiyo kwa zaidi ya asilimia 60 ya idadi ya watu katika nchi hizo, Morocco asilimia 48, na Tunisia, Comoros na Cape Verde zimetoa chanjo kwa asilimia 20 ya wananchi wao.

Mwezi Septemba, chanjo milioni 23 za COVID-19 ziliwasili Afrika, ikiwa ni ongezeko la asilimia 10 kuliko mwezi Juni, hata hivyo, ni watu milioni 60 tu katika bara hilo wamepata chanjo kamili mpaka sasa.